ckc 1

Vituo vyetu viwili vya jamii vimeanzishwa kwa watu wa Arumeru ili kupata teknolojia ya habari na mawasiliano.

Kwa ajili hii tunatoa huduma mbalimbali:

  • kozi za kompyuta
  • kozi za kiingereza
  • huduma za kuprint,laminesheni,kopi na kuskani
  • huduma ya mtandao
  • kuandika na kutuma barua pepe n.k

Malengo yetu

  • Kufanya ckc kituo cha elimu bora ndani ya wilaya ya Meru
  • Kufundisha na Kukuza huduma ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa watoto na watu wazima
  • Kuongeza uwezo wa elimu ya teknolojia na mawasiliano kwa jamii
  • Kuboresha maisha kwa jamii

HISTORIA

Kituo kikubwa cha ckc, CKC 1, ambacho kiko kwenye kijiji cha king’ori ,kilianzishwa na World Vision mwaka 2011, kikiwa kimefadhiliwa na mfadhili kutoka ujerumani.sherehe ya uzinduzi ilifanyika mwezi wa pili mwaka 2012,pamoja na world vision na familia ya mfadhili. Uanzishwaji wa CKC 2 (Kikatiti) na CKC 3 (Leguruki) ukafuata hatua kwa hatua.mwezi wa tisa 2014, world vision walijitoa kwenye mradi na majengo yote matatu pamoja na mali zote walikabidhiwa CBO Kikulunge. Kutoka hapo kampuni inayojiendesha bila faida,CKC King’ori imekua ikiendelea kuhakikisha kuwa huduma zinaendelea. Kwa wakati huu huduma za uendeshaji zinasaidiwa na shirika la kijerumani, Schick’sche Familienstiftung lakini lengo hasa ni kuifanya CKCs ijitegemee kabisa iondokane na ufadhili wa nnje. Japokuwa mwaka 2018 mwezi wa nane kituo cha CKC 2 kilifungwa. Ili kufikia lengo la vituo hivi kujiendesha vyenyewe, tunaendesha kituo cha CKC 1 na CKC 3 kwanza .

Wasiliana nasi: HAPA